Mtendaji Mkuu
Dkt. Stella Bitanyi
Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ni Wakala ya Serikali chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyoanzishwa kwa Sheria ya Wakala za Serikali Na. 245 (iliyofanyiwa marekebisho Mwaka 2009) na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali la tarehe 9 Machi 2012. Wakala ilizinduliwa rasmi tarehe 11 Ju...
Karibu
Mtendaji Mkuu
Dkt. Stella Bitanyi
Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ni Wakala ya Serikali chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliyoanzishwa kwa Sheria ya Wakala za Serikali Na. 245 (iliyofanyiwa marekebisho Mwaka 2009) na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali la tarehe 9 Machi 2012. Wakala ilizinduliwa rasmi tarehe 11 Julai, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi. Wakala hii ilitokana na kuunganishwa kwa iliyokuwa Maabara Kuu ya Mifugo (CVL), Vituo vya Kanda vya Uchunguzi na Utambuzi wa Magonjwa ya Mifugo (VICs), Taasisi ya Utafiti wa Ndorobo (TTRI) Tanga na Kituo cha Utafiti wa Ndorobo (TTRC) Kigoma.
Makao Makuu ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) yapo Temeke, eneo la Veterinari, jijini Dar es Salaam. Pamoja na Makao Makuu, pia kuna Vituo viwili vya Wakala ambavyo ni Maabara Kuu ya Mifugo (Central Veterinary Laboratory, CVL) na Kituo cha Magonjwa ambukizwa na Bioteknolojia (Centre for Infectious Diseases and Biotechnology, CIDB) vilivyoko katika eneo hilo. Vituo hivi ni Maabara za rufaa upande wa mifugo ambapo hupokea sampuli kutoka maabara za Kanda ili kufanya vipimo vya utambuzi wa vimelea vya magonjwa kwa kutumia vipimo vya ngazi za juu zaidi tofauti na vinavyofanywa na maabara za Kanda.
Wakala ina vituo vya kikanda 11 ambavyo hutekeleza majukumu mbalimbali ya Wakala katika maeneo yao. Vituo hivyo ni Taasisi ya Chanjo Tanzania (TVI) - KIBAHA-PWANI, TVLA-DODOMA , TVLA-IRINGA, TVLA-MWANZA, TVLA-ARUSHA, TVLA-TABORA, TVLA- MTWARA, TVLA-SUMBAWANGA, TVLA- MEATU - SIMIYU, Kituo cha utafiti wa magonjwa yaenezwayo na wadudu kwenye mifugo – VVBD - KIGOMA pamoja na Kituo cha utafiti wa magonjwa yaenezwayo na wadudu kwenye mifugo - VVBD- TANGA