SUMBAWANGA

TVLA SUMBAWANGA

 

Kituo cha TVLA Sumbawanga kinapatikana katika barabara ya Mahakama Kuu katikati ya Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na Ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga

 

MAENEO YANAYOHUDUMIWA

Kituo hiki cha TVLA - Sumbawanga kinahudumia mikoa ya Rukwa, Katavi na Songwe ambayo ina jumla ya Halmashauri 13.

 

SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA TVLA SUMBAWANGA

Kituo cha TVLA Sumbawanga kwa sasa kinaweza kufanya uchunguzi na utambuzi  wa baadhi ya magonjwa ya wanyama ambayo ni pamoja na matatizo ya minyoo wa aina zote (Helminthology), Magonjwa yasababishwayo na vimelea vya kwenye damu (Haemo-parasites), Bacteriology (Culture), Ugonjwa wa Kutupa mimba (Brucellosis), Ugonjwa wa Kimeta (Anthrax),  homa ya matumbo kwa kuku (Salmonellosis), Kichaa cha Mbwa (Rabies). Pia katika utambuzi wa magonjwa tunafanya upasuaji wa mizoga (Postmortem) kwa wanyama wa aina zote.