service image

Viuwatilifu ni sumu zinazotumika kuangamiza wadudu waenezao magonjwa na kusababisha usubufu ili kulinda afya ya wanyama. Nchini Tanzania vifo vingi vya ng’ombe husababishwa na magonjwa yanayoenezwa na kupe na mbung’o ikiwa ni pamoja na ndigana kali, ndigana baridi, mkojo mwekundu (babesiosis), maji moyo (heart water) na nagana inayoenezwa na mbung’o. TVLA inatekeleza jukumu la kusajili, kupima na kudhibiti viuatilifu vya mifugo nchini kazi ambayo inafanywa na maabara kuu ya veterinari iliyopo Temeke. Katika kutekeleza jukumu hilo wakala inasajili viuatilifu vipya nchini, inatoa vibali vya kuingiza viuatilifu vya mifugo vilivyosajiliwa nchini na inatoa vibali vya kuuza viuatilifu nchini kwa wenye maduka ya jumla na rejareja. Vilevile, Wakala inatoa vibali vya kufungasha viuatilifu na vibali vya kuzalisha kwa viwanda vya kuzalisha viuatilifu. Wakala inahakiki ubora wa viuwatilifu vinavyotengenezwa nchini, vinavyoingizwa na kufanya ufuatiliaji wa viuwatilifu vilipo sokoni ili kudhibiti matumizi na ubora wa viatilifu hivyo. Vilevile, maabara inapokea sampuli za majosho kwa ajili ya kujiridhisha na ubora na ufanisi wa dawa inayotumika kuogesha wanyama kwenye josho na kushauri kamati za majosho kuhusu matumizi sahihi ya viuatilifu vilivyo kwenye soko.

 

Kwa usajili ingia .portal