CHANJO DHIDI YA HOMA YA MAPAFU YA NG'OMBE (CBPP)

CHANJO YA BOVIVAC

 

BOVIVAC in chanjo iliyotengenezwa kwa vimelea hai vilivyofubazwa vya Mycoplasma mycoides subspecies Mycoides strain T1/44 kwa ajili ya kuchanja ng’ombe dhidi ya ugonjwa wa homa ya mabafu. Homa ya mapafu ya ng’ombe inayosababibishwa na vimelea vya Mycoplasma mycoides subsp. hushambulia mapafu na kusababisha homa na ugumu wa kupumua kwa ngombe. BOVIVAC inazalishwa kulingana na viwango vya ubora chini ya muongoza wa viwango vya ubora wa ISO 9001:2015 pamoja na viwango na miongozo ya Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH).

 

 

 

Mnyama mlengwa na jinsi ya kutumia

 

Chanjo ya BOVIVAC inatumika kuchanja ng'ombe wenye umri wa miezi sita na kuendelea na itolewa kwa ng'ombe ambaye hana dalili zozote cha ugonjwa. Kidonge kimoja cha chanjo ya BOVIVAC kichanganywe kwenye mililita 100 za kimiminika maalumu kinachotolewa na chanjo hii (sawa na dozi 100). Ng'ombe achomwe mililita 1 ya chanjo chini ya ngozi iliyo nyuma ya bega kwa kutumia sindano husika. Chanjo iliyoandaliwa ihifadhiwe kwenye ubaridi (cool box) na itumike ndani ya saa moja. Chanjo iliyobaki yaweza kutumika ndani ya siku 7 ikiwa tu imehifadhiwa kwenye jokofu (2℃-8℃) vinginevyo iharibiwe kwenye majimoto. Hakikisha umesafisha kizibo kwa kutumia 70% alcohol kabla ya kuchukua chanjo kwenye chupa. Wakati wa zoezi la uchanjaji, chanjo iliyoko ndani ya bomba la kuchanjia, isikae zaidi ya dakika kumi nje ya ubaridi.

 

Uhifadhi na mwonekano

 

Chanjo ya BOVIVAC iliyoko katika hali ya kidonge hutunzwa kwenye ubaridi mkali wa nyuzi joto -20℃ chini ya sifuri (minus 20℃) na ikihifadhiwa katika ubaridi huu hudumu kwa muda wa miaka miwili. Kimiminika maalum cha kuchanganyia/kuyeyushia kidonge huhifadhiwa kwenye nyuzi joto 2°C - 8°C.

 

Usafirishaji

 

Chanjo isafirishwe katika mnyororo wa ubaridi kwa kuwekwa ndani ya kasha la baridi lenye barafu (2°C -8℃) mpaka wakati wa kumchoma mnyama.

 

Mambo ya kuzingatia

 

  • Uchanjaji wa chanjo hii ufanywe na Daktari wa wanyama au Daktari msaidizi waliosajiliwa na Baraza la Veterinary Tanzania (VCT);
  • Usichanje ng’ombe wagonjwa;
  • Usitumie chanjo kama sili imevunjwa;
  • Tikisa chupa kabla ya kujaza bomba la sindano;
  • Usiweke chanjo iliyochanganywa kwenye jua;
  • Mnyama anaweza kupata kidonda kwenye eneo lililochomwa chanjo, ikitokea mtibu kwa kutumia sindano ya tylosin na kusafisha kidonda mpaka kipone;
  • Rudia chanjo kila baada ya miezi 12
  • Mabomba ya sindano, gloves na chupa vilivyotumika viteketezwe kwa moto.

 

Kwa msaada zaidi wa kitalaam wasiliana na tabibu wa wanyama alie karibu nawe.

 

BOVIVAC inazalishwa na:

TAASISI YA CHANJO TANZANIA (TVI),

Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA),

S.L.P. 30137,

Kitalu Na. 34, Pangani area, Kibaha.

Simu: 0733 282 032/0785 553 260

Baruapepe: tvi@tvla.go.tz

Kibaha – TANZANIA.