CHANJO DHIDI YA UGONJWA WA KUTUPA MIMBA KWA NG'OMBE

BRUCELLOSIS 19 VACCINE

 

BRUCELLOSIS 19 ni chanjo inayoandaliwa kwa kutumia vimelea hai vilivyopunguzwa makali vya Brucella abortus iliyo kwenye mfumo wa kidonge kwa ajili ya kuchanja ng’ombe dhidi ya Ugonjwa wa Kutupa Mimba. Ugonjwa wa kutupa mimba ni ugonjwa wa kuambukiza wa wanyama unaosababishwa na vimele vya Brucella spicies. Binadamu anaweza kupata ugonjwa huu kwa kugusana na wanyama wenye ugonjwa au bidhaa za wanyama. BRUCELLOSIS 19 inazalishwa kulingana na viwango vya ubora chini ya muongoza wa viwango vya ubora wa ISO 9001:2015 pamoja na viwango na miongozo ya Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH).

 

Mnyama mlengewa na jinsi ya kutumia

 

BRUCELLOSIS 19 inatumika kuchanja ng’ombe ambaye haumwi dhidi ya Ugomjwa wa Kutupa Mimba. Chanjo ambayo huwa ni kidonge inabidi iyeyushwe kwa kutumia kimiminika chenye ujazo wa mililita 50 kinachotolewa na chanjo hii mchanganyiko unaotosha ng’ombe 25 (dozi 25). Uchanganyaji unafanywa kwa kuchanganya mililita 5 za kimiminika kilichopozwa kwenye jokofu na kidonge cha chanjo kilicho kwenye chupa yake ikifuatiwa na kutikisa kwa uangalifu. Mchanganyiko unaopatikana urudishwe tena kwenye chupa ya kimiminika. Chukua kiasi kidogo cha mchanganyiko huo utumie kusuuza chupa iliyokuwa na kidonge alafu mchanganyiko urudishwe kwenye chupa kubwa na chanjo itakuwa tayari kwa matumizi. Tikisa chupa yenye mchanganyiko taratibu, vuta chanjo kwenye sindano safi na uchome mililita 2 za chanjo chini ya ngozi. Weka chanjo iliyotayari kwa matumizi kwenye ubaridi na kwenye kivuli. Rudia uchanjaji kila mwaka.

 

Uhifadhi na muonekano

 

Chanjo hii iko kwenye mfumo wa kidonge ikiambatana na kimiminika cha kuchanganyia sawa na dozi 25. Hifadhi kidonge cha chanjo kwenye jotoridi la 20℃ chini ya sifuri. Ikihidahiwa kwenye jotoridi hili inaweza kuwekwa kwa miezi 24 kabla ya matumizi. Chanjo iliyochanganywa itumike ndani ya saa moja baada ya kuchanganywa.

Usafirishaji

 

Safarisha chanjo hii kwenye mnyororo wa ubaridi kwa kutumia kasha la kuhifadhi baridi lenye barafu (2℃ - 8℃) mpaka itakapo tumika.

 

Mambo ya kuzingatia

 

  • Uchanjaji wa BRUCELLOSIS 19 ufanywe na Daktari wa wanyama au Daktari msaidizi waliosajiliwa na baraza la veterinary Tanzania (VCT);
  • Usichanje wanyama wagonjwa;
  • Wanyama wachanjwe kila baada ya miezi 12;
  • Usitumie chanjo kama sili imeharibika;
  • Chanja wanyama wenye umri wa miezi sita (6) au zaidi na
  • Chanjo iliyobaki iharibiwe kwenye maji ya moto au kwenye bleach.

 

Kwa msaada zaidi wa kitalaam wasiliana na tabibu wa mifugo alie karibu nawe.

 

BRUCELOSIS 19 inazalishwa na:

TAASISI YA CHANJO TANZANIA (TVI),

Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA).

S.L.P. 30137,

Kitalu Na. 34, Pangani area, Kibaha.

Simu: 0733 282 032/0785 553 260

Baruapepe: tvi@tvla.go.tz

Kibaha – TANZANIA.