service image

Vyakula vya mifugo

Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania ni maabara inayotambulika kwa uchambuzi wa vyakula vya wanyama inayofanya kazi chini ya sharia ya Nyanda za Marisho na Rasilimali ya Vyakula vya Mifugo sura namba 180 ya mwaka 2010 na kanuni zake za mwaka 2013.Maabara ya vyakula vya wanyama ya Wakala inatoa huduma tofauti za uchambuzi wa vyakula vya wanyama zitakazokusaidia biasahara au shamba lako kuzalisha kwa faida. Wakala ina maabara yenye wataalam na vifaa vya kisasa kwa ajili ya uchambuzi wa ubora wa vyakula vya wanyama ikiwemo Energy Dispersive X-ray Fluorescence spectrometer (EDXRF) kwa ajili ya uchambuzi wa madini kwenye vyakula and Near-InfraredSpectrometer (NIRS) kwa ajili ya uchambuzi wa virutubisho.Maabara ina uwezo wa kuchambua viwango vya nishati, protini, amino asidi kwa kutumia NIRS, uchambuzi wa aina na kiwango cha madini kwa kutumia EDXRF, ubora wa soya inayotumika kuzalisha chakula cha wanyama kwa kutumia kipimo cha urease activity index na kiwango cha udongo (mchanga) kwenye malighafi za kuzalisha chakula cha mifugo kwa kutumia kipimo cha acid insoluble ash.Uchambuzi wa vyakula vya mifugo ni hitaji muhimu katika kuandaa chakula bora cha wanyama na ufanisi katika kufanya tathmini ya mahitaji ya nyongeza ya virutubisho muhimu kwa ajili ya kuongeza ufanisi kwenye uzalishaji wanyama. Hivyo, mkusanyiko wa njia za uchambuzi zinazotumika kwenye maabara zinalenga kutoa taarifa za virutubisho na ubora zinazohotajika katika kufanya maamuzi sahihi katika utengenezaji vyakula vya mifugo vyenye ubora. Vilevile, uchambuzi wa vyakula vya wanyama na malighafi zinazotumika kutengeneza vyakula vya wanyama ni muhimu kuhakikisha wazalishaji wa vyakula vya wanyama wanazalisha vyakula vyenye ubora vinavyokidhi mahitaji ya uzalishaji wa wanyama.