vaccine image

Chanjo ya Kimeta in chanjo ya vimelea hai vya Bacillus anthracis strain 34 F 2 (Sterne) vilivyofubazwa makali yenye uwezo wa kukinga wanyama dhidi ya ugonjwa wa Kimeta. Kimeta ni ugonjwa unaathiri wanyama wote wenye damu moto (ikijumuisha ng’ombe, punda, kondoo, mbuzi, farasi) akiwemo binadamua unaosababishwa na kimelea anayeitwa Bacillus anthracis. Chanjo ya Kimeta inazalishwa kulingana na vijwango vya ubora chini ya muongoza wa viwango vya ubora wa ISO 9001:2015 pamoja na viwango na miongozo ya Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH).