Maabara Kuu ya Mifugo

OFISI ZA MAKAO MAKUU

WAKALA YA MAABARA YA VETERINARI TANZANIA

Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ni Wakala ya Serikali chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.  Ofisi za Makao makuu ya Wakala yapo eneo la Temeke-Dar es Salaam pembezoni mwa barabara ya Mandela. Makao Makuu ya Wakala yana ofisi za Mtendaji Mkuu, Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo, Mameneja na watumishi wote wa Makao Makuu.

Anwani

Mtendaji Mkuu,

S.L. P 9254,

Majengo ya Veterinari, 131 Barabara ya Nelson Mandela,

Temeke- Dar es Salaam,Tanzania

Simu: +255 22 2861152
Nukushi: +255 22 2864396
Baruapepe: info@tvla.go.tz

 

MAABARA KUU YA VETERINARI (CVL)

 

Maabara kuu ya Veterinari ni mojawapo ya vituo vya Wakala ambayo ipo katika eneo la Temeke, Dar es Salaam, pembezoni mwa barabara ya Nelson Mandela. Hii ni maabara ya rufaa ya wanyama nchini katika uchunguzi na utambuzi wa magonjwa ya wanyama yanayosababishwa na bacteria, fangasi, protozoa na minyoo; na kufanya utambuzi wa wadudu waenezao magonjwa ya wanyama kama vile kupe, mbung’o na mbu. Maabara hii pia inafanya uhakiki wa ubora wa vyakula vya wanyama na kupima viuatilifu vya wanyama kuhakiki ubora na kufanya usajili wa viuatilifu vipya. Kituo hiki kina ithibati ya kimataifa (ISO/IEC 17025:2017) ya utambuzi wa magonjwa ya wanyama.

 

Kwa mawasiliano;

 

Meneja,

Maabara Kuu ya Veterinari,

S.L. P 9254,

Majengo ya Veterinari, 131 Barabara ya Nelson Mandela,

Temeke- Dar es Salaam,Tanzania

Simu: +255 22 2861152
Nukushi: +255 22 2864396
Baruapepe: cvl@tvla.go.tz