vaccine image

CAPRIVAC ni chanjo iliyotengenezwa kwa vimelea vilivyouwawa inayotumika kuchanja mbuzi dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu. Ugonjwa wa Homa ya Mapafu ya Mbuzi ni ugonjwa hatari wa mbuzi unaosababishwa na vimelea vya Mycoplasma capricolum subspecies capripneumoniae (Mccp). CAPRIVAC inazalishwa kulingana na vijwango vya ubora chini ya muongoza wa viwango vya ubora wa ISO 9001:2015 pamoja na viwango na miongozo ya Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH).