CHANJO DHIDI YA UGONJWA WA KIMETA KWA NG’OMBE, MBUZI NA KONDOO

CHANJO YA KIMETA

 

Chanjo ya Kimeta in chanjo ya vimelea hai vya Bacillus anthracis strain 34 F 2 (Sterne) vilivyofubazwa makali yenye uwezo wa kukinga wanyama dhidi ya ugonjwa wa Kimeta. Kimeta ni ugonjwa unaathiri wanyama wote wenye damu moto (ikijumuisha ng’ombe, punda, kondoo, mbuzi, farasi) akiwemo binadamua unaosababishwa na kimelea anayeitwa Bacillus anthracis. Chanjo ya Kimeta inazalishwa kulingana na vijwango vya ubora chini ya muongoza wa viwango vya ubora wa ISO 9001:2015 pamoja na viwango na miongozo ya Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH).

 

Mnyama mlengwa na jinsi ya kutumia

 

Chanjo ya Kimeta inatumika kujanja ng’ombe, mbuzi na kondoo ambao hawaonyeshi dalili za ugonjwa wowote na wenye umri wa miezi sita (6) au zaidi. Tumia sindano na bomba kuchoma mililita 1 ya chanjo na hakikisha unatikisa chupa kabla ya kuvuta chanjo kwa sindano kutoka kwenye chupa. Choma mnyama chini ya ngozi nyuma ya bega au eneo la shingo baada ya kumdhibi mnyama vyema. Wanyama wachanjwe kila baada ya miezi 12.

 

Uhifadhi na mwonekano

 

Chanjo ya kimeta iko kwenye kimiminika cha rangi ya kijivu kilichopauka kwenye chupa ya kioo ya kahawia ya mililita 100 ambazo ni sawa na dozi 100. Hifadhi chanjo ya Kimeta kwenye ubaridi wa 2℃ – 8℃. Chanjo ya Kimeta isiwekwe kwenye sehemu ya kugandisha. Chanjo ya Kimeta ikiwekwa kwenye ubaridi wa 2℃ - 8℃ inabaki na ubora wake kwa mwaka mmoja (miezi 12).

 

Usafirishaji

 

Chanjo ya Kimeta isafirishwe kwenye mnyororo wa ubaridi kwa kutumia kasha la kutunza ubaridi lenye barafu kuhakikisha chanjo inabaki kwenye ubaridi wa 2℃ - 8℃ mpaka itakapotumika.

 

Mambo ya kuzingatia

 

  • Uchanjaji dhidi ya Kimeta ufanywe na Daktari wa wanyama au Daktari msaidizi waliosajiliwa na baraza la veterinary Tanzania (VCT);
  • Usichanje wanyama wagonjwa;
  • Wanyama wachanjwe kila baada ya miezi 12;
  • Usitumie chanjo kama sili imeharibika;
  • Chanja wanyama wenye umri wa miezi sita (6) au zaidi na
  • Chupa zilizoisha chanjo, sindano, gloves na vifaa vyote vilivyotumika vichomwe kwa moto mkali au visafishe na kipukusi kabla ya kuvitupa au kuvichoma.

 

Kwa msaada zaidi wa kitalaam wasiliana na tabibu wa wanyama alie karibu nawe.

 

Chanjo ya Kimeta inazalishwa na:

TAASISI YA CHANJO TANZANIA (TVI),

Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA).

S.L.P. 30137,

Kitalu Na. 34, Pangani area, Kibaha.

Simu: 0733 282 032/0785 553 260

Baruapepe: tvi@tvla.go.tz

Kibaha – TANZANIA.