Arusha

Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania kanda ya Kaskazini-Arusha, ni moja ya Maabara ya Kanda inayotoa huduma ya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo na Wanyama pori katika Mikoa mitatu ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara. Kituo kina wajibu wa kutoa uchunguzi wa magonjwa ya kuambukiza (zoonotic), ufuatiliaji wa magonjwa na kushirikiana na miradi ya wafadhili kufanya utafiti wa magonjwa ya Wanyama. Maabara imegawanyika katika sehemu kuu 6, nazo ni: Protozoology, Pathology, Helminthology, Serology, Bacteriology and Molecular biology. Kituo pia kina jukumu kubwa la kutoa mafunzo ya vitendo (field practical) kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kati vya mifugo, wataalamu wa mifugo (paravet) na madaktari wa mifugo (veterinarian). Kituo pia kinahudumia idadi kubwa ya hifadhi maarufu za Taifa zilizoko katika kanda kwa kufanya uchunguzi wa magonjwa ya wanyama pindi mlipuko unapotokea. Hifadhi hizo ni Pamoja na Serengeti, Ngorongoro, Manyara, Arusha na Tarangire Aidha kituo pia kinatoa ushauri wa uthibiti wa magonjwa ya mifugo, Wanyama pori na usambasaji/ kuuza chanjo zinazozalishwa na Taasisi ya chanjo Kibaha (TVI),  chanjo hizo ni Pamoja na Mdondo (I-2) kwa kuku, Kimeta, Chambavu (BQ), Tecoblax, Mapafu ya ngombe (CBPP), mapafu ya mbuzi (CCPP) na kutupa mimba (brucellosis) S -19).

Kwa mawasiliano unaweza kutupata kwa annuani ifuatayo:

Ofisi ya Kanda,

Simu +255 27 2545402
Nukushi: +255 27 2545402
baruapepe: tvla.arusha@tvla.go.tz
Sanduku la posta: 1068 Arusha, Tanzania.

Barabara ya Africa Mashariki,

Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania,