service image

Huduma za utambuzi wa magonjwa

Wakala ya Maabara ya Verinari Tanzania (TVLA) imepewa mamlaka ya kufanya uchunguzi wa magonjwa nchini. Wakala ina maabara mbili za rufaa za utambuzi wa magonjwa ya wanyama zinzotambulika kimataifa (ISO/IEC 17025:2017) ambazo ni Maabara Kuu (CVL) na Kituo cha Magonjwa Yanayoambukiza na Bioteknoloji (CIDB) vyote vinapatikana Dar es Salaam.  Pamoja na vituo hivi vya rufaa, Wakala ina vituo vingine kumi na moja (11) vinavyopatikana katika kanda mbalimbali za Tanzania vyenye uwezo tofauti wa utambuzi wa magonjwa. Wakala huwa inapokea sampuli za wanyama wa aina mbalimbali katika vituo vyake vyote kumi na tatu (13) kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa.

 

Maabara zilizo chini ya Wakala zinatumia njia mbalimbali za utabuzi wa magonjwa zikiwemo hadubini serolojia na upimaji wa vinasaba (PCR). Maabara zina uwezo wa kuotesha bacteria na kuwatambua kwa kutumia njia za kawaida na kwa kutumia vifaa za vya kisasa (V-TEK MS), kutambua usugu wa dawa kwa bacteria kwa njia za kawaida na kwa kutumia vifaa vya kisasa (V-TEK 2 Compact), utambuzi wa ugonjwa wa kutupa mimba kwa kutumia njia za serolojia na vinasaba, ugonjwa wa mapafu ya ng’ombe na mbuzi kwa kutumia serojia, ugonjwa wa kimeta kwa kutumia vinasaba, utambuzi wa vimelea vya kwenye damu, wadudu na minyoo kwa njia ya hadubini na utambuzi wa magonjwa kupitia uchunguzi wa mizoga. Kituo cha Magonjwa Yanayoambukiza na Bioteknolojia ni maalum kwa ajili ya utambuzi wa magonjwa yanayosababishwa na virusi yakiwemo ugonjwa wa Miguu na Midomo, Sotoka ya Mbuzi na Kondoo, Kichaa cha Mbwa, Mdondo, Mafua Makali ya Ndege na Homa ya Nguruwe kwa kutumia njia mbalimabili zikiwemo serolojia na vinasaba. Huduma ya utambuzi wa magonjwa kwa njia ya vinasaba inapatikana kwenye maabara zote mbili za rufaana maabara nne (4) za kanda zinazopatina Arusha, Mwanza Dodoma and Iringa.