service image

Ushauri na mafunzo kwenye afya ya wanyama na lishe ni miongoni mwa huduma zinazotolewa na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA). Wataalamu walioajiriwa na Wakala wana jukumu la kutoa huduma mbalimbali za ushauri na mafunzo kwa mtu mmoja mmoja na makundi mbalimbali kulingana na mamlaka ya Wakala. Ushauri na mafunzo yanayotolewa na Wakala yako katika maeneo ya kukinga na kuthibiti magonjwa yanayosambazwa na wadudud, utambuzi wa magonjwa, uhifadhi na matumizi sahihi ya chanjo, uchanganyaji wa chakula cha wanyama na ubora wa chakula cha wanyama, mahitaji ya kisheria ya uingizaji nchini, kufungasha na kuzalisha viuatilifu vya wanyama, matumizi sahihi ya viuatilifu vya wanyama na usimamizi wa ubora kwenye maabara za utambuzi wa magonjwa ya wanyama. Vilevile, Wakala inatoa huduma za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wanaosoma teknolojia ya maabara za veterinary na kozi zingine za sayansi kutoka vyuo vikuu na vyuo vya kati ndani na nje ya nchi.Zaidi ya hayo, Wakala inatoa nafasi kwenye maabara zake kwa wanafunzi wa uzamili na uzamivu kufanya tafiti zao na kutoa huduma ya usimamizi wa wanafunzi hao.Wakala inatoa ushauri na mafunzo kwenye ngazi za mfugaji mmoja mmoja, makampuni, taasisi binafsi na za umma, mashiriki ya kitaifa na kimataifa.