vaccine image

BRUCELLOSIS 19 ni chanjo inayoandaliwa kwa kutumia vimelea hai vilivyopunguzwa makali vya Brucella abortus iliyo kwenye mfumo wa kidonge kwa ajili ya kuchanja ng’ombe dhidi ya Ugonjwa wa Kutupa Mimba. Ugonjwa wa kutupa mimba ni ugonjwa wa kuambukiza wa wanyama unaosababishwa na vimele vya Brucella spicies. Binadamu anaweza kupata ugonjwa huu kwa kugusana na wanyama wenye ugonjwa au bidhaa za wanyama. BRUCELLOSIS 19 inazalishwa kulingana na viwango vya ubora chini ya muongoza wa viwango vya ubora wa ISO 9001:2015 pamoja na viwango na miongozo ya Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH).