vaccine image

Chanjo ya Chanbavu ni chanjo inayozalishwa kwa vimelea vilivyouawa inayokinga ng’ombe na kondoo dhidi ya ugonjwa wa Chambavu. Chambavu ni ungonjwa unaosababisha vifo kwenye ng’ombe na kondoo unaosababishwa na kimelea aitwaye Clostridium chauvoei. Chanjo ya Chambavu inazalishwa ikiwa ni sumu ya kimelea cha Clostridium Chauvoei (Clostridium Chauvoeicytotoxin A - CctA proteins) toka kwenye kimelea kilichouawa kwa fomaliniChanjo ya Chambavu inazalishwa kulingana na viwango vya ubora chini ya muongozo wa viwango vya ubora wa ISO 9001:2015 pamoja na viwango na miongozo ya Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH).