TVLA yapatiwa mafunzo ya PIPMIS na PEPMIS
TVLA yapatiwa mafunzo ya PIPMIS na PEPMIS

Watumishi wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) wamepatiwa mafunzo juu ya mifumo mipya ya Upimaji utendaji kazi kwa Taasisi (PIPMIS) na Mfumo wa upimaji utendaji kwa wafanyakazi wa umma (PEPMIS).

Mafunzo hayo yametolewa leo Disemba 08, 2023 na wataalam kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma na Utawala Bora yaliyoongozwa na Bwana Jones Kabwato kwa lengo la kutatua changamoto zilizokuwepo kwenye mfumo wa OPRAS, na PIPMIS umeundwa kutatua changamoto zilizokuwepo kwenye mfumo wa IPCS.

Mfumo huo wa PEPMIS utapunguza na kuondoa matumizi ya karatasi, kuongeza uwazi katika usimamizi wa watumishi na kuondoa upendeleo na uonevu katika upimaji na utendaji kazi kwa watumishi

Mafunzo hayo yamefunguliwa na kufungwa na Mtendaji Mkuu wa TVLA Dkt. Stella Bitanyi katika ukumbi wa TVLA uliopo Temeke Veterinari pamoja na kwenye ofisi zote za kanda za TVLA zilizopo Dodoma, Arusha, Tanga, Mwanza, Meatu-Simiyu, Tabora, Kigoma, Sumbawanga, Iringa na Mtwara kwa njia ya Mtandao.

Mafunzo juu ya mifumo mipya ya Upimaji utendaji kazi kwa Taasisi (PIPMIS) na Mfumo wa upimaji utendaji kwa wafanyakazi wa umma (PEPMIS) yamewahusisha Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo, Wakuu wa Sehemu, Mameneja wa Kanda pamoja na wasaidizi wao.