TVLA Mshindi wa Kwanza Marathon Wiki ya Maziwa Morogoro.

Na Daudi Nyingo
Hayo yamebainishwa na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Ndg. Abdul Rajabu Mhinte alipokuwa akigawa tuzo kwa washishindi wa mbio za marathon kilometa 5 na 10 zilizofanyika mkoa wa Morogoro Mei 31, 2025 kwenye uwanja wa Zimamoto ambapo TVLA ambapo Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ikiwakilishwa na Afisa Masoko Bw. Fihiri Mbawala Kuibuka Mshindi wa kwanza.
Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) imeibuka mshindi wa kwanza kwenye Mbio za Marathon umbali wa kilometa 5 zilizoandaliwa na Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) kwenye maadhimisho ya wiki ya Maziwa yanayofanyika mkoani Morogoro kwenye uwanja wa Zimamoto ambapo TVLA iliwakilishwa na Afisa Masoko Bw. Fihiri Mbawala.
Mashindano ya mbio za Marathon mkoani Morogoro yamenogesha Wiki ya Maziwa kwa kuhamasisha jamii kutumia maziwa kama chakula kwani yana virutubisho vingi muhimu vinavyohitajika kwenye mwili wa binadamu.
Akikabidhi zawadi kwa washindi Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Ndg. Abdul Rajabu Mhinte ameipongeza Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) kuandaa maonesho ya wiki ya maziwa kwa mwaka 2025 ambayo yamekwenda sambamba na mashindano ya mbio za marathon yajulikanayo kama Milk Week Marathon vilevile amewapongeza wote walioshiriki mashindano hayo.
“Tuendelee kuikuza Sekta ya Maziwa ili ifikie lengo lililokusudiwa kwa maana ya uzalishaji na hata matumizi yake. Tuweke misngi bora ya maziwa kuwa chakula muhimu katika vyakula vyetu vya kila siku kinachojaziliza lishe zetu na sio chakula cha kutumia katika wakati maalumu.”
“Pamoja na kwamba maziwa ni lishe, ila ni sehemu ya uchumi wa maisha yetu, tuongeze uzalishaji ili yawe sehemu ya kukuza uchumi.” Alisema Bw. Mhinte.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kunywa maziwa kila siku ili kuimarisha afya zao.