NAIBU WAZIRI MKUU AVUTIWA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA TVLA
NAIBU WAZIRI MKUU AVUTIWA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA TVLA

Na Daudi Nyingo

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko amevutiwa na huduma zinazotolewa na Wakala ya Maabala ya Veterinari Tanzania (TVLA) alipotembelea banda la TVLA siku ya kilele cha Maonesho na Mnada wa Mifugo 2024 yaliyofanyika kwenye shamba la Mkonge la Highland Estate Chalinze Ubena Zomozi Mkoa wa Pwani Juni 16, 2024.

Akiongea kwa niaba ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Dkt. Benezeth Malinda alisema kuwa majukumu makubwa ya TVLA ni pamoja na kufanya utafiti wa magonjwa ya wanyama, kufanya uchunguzi wa magonjwa ya wanyama, kuzalisha na kusambaza chanjo za magonjwa ya Mifugo ambapo hadi sasa TVLA inazalisha aina 7 za chanjo.

Sambamba na hayo Dkt. Malinda aliongeza kuwa, mkakati wa Wizara kwa kushirikiana na TVLA imepanga hadi kufikia mwaka 2030 itakuwa inazalisha Chanjo 13 za kipaumbele na hadi kufikia sasa TVLA tayari imeshanunua magari ya mfumo wa baridi ambayo yanasambaza chanjo ambazo zimeshaanza kuzalishwa ili kuwafikia wafugaji kote nchini.

Mhe. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 29 kwa ajili ya kuendesha kampeni ya chanjo kitaifa kwa lengo la kuhamasisha wafugaji kuchanja Mifugo yao ili kuzuia isishambuliwe na magonjwa kwani kuchanja Mifugo kutaongeza mazao ya Mifugo kukizi soko la nje ya nchi. Alisema Dkt. Malinda

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko aliongozana na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexandar Mnyeti (MB), Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe, Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Daniel Mushi pamoja na viongozi waandamizi wa Wizara.

MWISHO